Azam yazipotezea Simba, Yanga

KOCHA MSAIDIZI WA AZAM FC, IDDI CHECHE.

BAADA ya timu yake kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA (Tanzania), Kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddi Cheche, amesema hana hofu na timu yoyote watakayokutana nayo kwenye hatua hiyo.

Azam imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Ndanda FC mabao 3-1 katika mechi ya hatua ya robo fainali iliyofanyika juzi usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Cheche alisema kuwa hana hofu yoyote kati ya timu hizo kongwe endapo atakutana nayo kwenye hatua hiyo inayofuata.

Hata hivyo, Yanga bado haijafuzu hatua hiyo, mpaka pale itakapovaana na Tanzania Prisons ifikapo Aprili 22 kwenye Uwanja wa Taifa jijini.

"Kikubwa tunamshukuru Mungu tumevuka hatua hii, tutaendelea kupambana ili tusonge mbele, tunafahamu kwenye Ligi Kuu tumeshapoteza mwelekeo, michuano hii ndiyo itatupa tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani endapo tutatwaa ubingwa," alisema Cheche.

Aliongeza kuwa kila mechi kwao ni zaidi ya fainali na wachezaji wake wanafahamu umuhimu wa nafasi ambayo wanaitafuta.

Azam FC imeendelea kukosa huduma ya nahodha wake, John Bocco, ambaye bado ni majeruhi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items