MDHIBITI na Makaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad, amebaini kuwapo kwa upungufu katika taarifa za fedha za vyama vya siasa, kikiwamo chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika ripoti yake ya mwaka 2015/16 iliyowasilishwa bungeni mjini hapa juzi, CAG Assad alisema CCM iliripoti mali za kudumu kwenye taarifa za fedha zenye thamani ya Sh. bilioni 36.869.
Hata hivyo, Prof. Assad alisema katika ripoti hiyo kuwa amebaini hakuna daftari la mali za kudumu, hivyo kushindwa kuthibitisha ukamilifu wa taarifa za mali za kudumu.
"Chama hakikufanya tathmini ya mali za kudumu, hivyo mali za kudumu kwenye taarifa za fedha zenye thamani ya Sh. 36,869,775,776 hazikuwa sahihi," anasema CAG Assad katika kitabu chake cha ukaguzi wa taarifa za hesabu za Serikali Kuu.
Katika ripoti hiyo, Prof. Assad pia anasema CCM haikutenganisha thamani ya ardhi na thamani ya hati za ukaguzi wa majengo kama viwango vya kimataifa vya kihasibu vinavyotaka (aya 58 of IAS 16), hivyo thamani ya majengo ya Sh. bilioni 9.809 yalijumuishwa na thamani ya ardhi ambayo inapanda thamani wakati majengo yanashuka thamani.
"Hatukuweza kupata taarifa za fedha kuhusu uwekezaji wa chama kwenye kampuni mbalimbali, hivyo kushindwa kujiridhisha na uwekezaji wenye thamani ya Sh. 10,879,571,868 uliowasilishwa kwenye taarifa za fedha," anasema CAG katika ripoti hiyo.
Anaongeza kuwa katika taarifa ya matumizi, alibaini Sh. bilioni 32.864 zilipelekwa kwenye taasisi zilizo chini ya chama, lakini taarifa za matumizi katika taasisi hizo hazikupatikana ili kujiridhisha na matumizi hayo.
Aidha, CAG Assad anasema matumizi yenye thamani ya Sh. milioni 82.4 yalikuwa na nyaraka pungufu, hivyo kushindwa kuthibitisha uhalali wake.
"Madai yenye thamani ya Sh. 137,582,752 kutoka CCM Kinondoni hayakuingizwa kwenye taarifa za fedha, hivyo kusababisha upungufu wa Sh. 137,582,752 kwenye taarifa za fedha," anasema.
Anaongeza: "Katika taarifa ya fedha, nyumba na majengo yenye thamani ya Sh. 80,000,000 viliwekwa pamoja, badala ya kutenganishwa kama viwango vya kimataifa ya uandaaji wa hesabu za umma (aya 74 ya IPAS 17) vinavyoagiza."
Mbali na CCM, Prof. Assad pia anabainisha kuwa Chama cha TLP hakikutunza vitabu vya uhasibu kama leja za matumizi, daftari la mapato na matumizi na la mali za chama kinyume cha kifungu cha 14(1)(b) cha Sheria ya Vyama vya Siasa.
Anasema kukosekana kwa kumbukumbu hizo kunasababisha uandaaji wa taarifa za fedha kukosa vyanzo vya uhakika na hivyo kufanya ukaguzi wa taarifa kukosa mtiririko, usahihi, uwazi na taarifa za uhakika.
CAG Assad anasema ruzuku iliyopokelewa kwenye akaunti ya benki haikuingizwa kwenye vitabu vya fedha na chama hicho hakikufanya usuluhishi wa kibenki, hivyo kushindwa kuthibitisha bakaa ya fedha kwenye taarifa ya fedha.
ACT WAZALENDO
CAG pia anasema Chama cha ACT Wazalendo hakikutunza vitabu vya fedha kama vile vitabu vya stakabadhi, daftari la fedha, daftari la leja na daftari la mali za kudumu kwa ajili ya taarifa za fedha kinyume na Kifungu cha 14(10)(a) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, hali iliyopunguza mawanda ya ukaguzi.
Anasema chama hicho kilikusanya mapato ya Sh. 498,730,000 kama michango ya wanachama, lakini ni Sh. 410,295,659 zilizoripotiwa kwenye taarifa za fedha, hivyo kupelekea upungufu wa Sh. 88,434,341 kwenye taarifa za fedha.
Anaongeza kuwa mapato yatokanayo na mauzo ya matangazo hayakuingizwa kwenye vitabu vya stakabadhi, lakini taarifa ya fedha ya mwaka ilikuwa na kiasi cha Sh. 2,191,341, hivyo kusababisha taarifa kuwa na makosa.
Pamoja na hayo, CAG Assad anasema taarifa za fedha zilionyesha Sh. 840,000 kama mapato yatokanayo na ada ya uchaguzi, lakini vitabu vya stakabadhi viliripoti Sh. 1,560,000, hivyo kusababisha kuwapo kwa pungufu ya Sh. 720,000.
Aidha, Prof. Assad anasema mali zenye za thamani ya Sh. 11,343,340 zilionyeshwa kwenye taarifa ya mtiririko wa fedha taslimu (Cash Flow), lakini hazikuonyeshwa kwenye mizania ya hesabu (Statement of Financial Position).
Kwa mwaka unaoishia Juni, 2015, CAG anasema ACT Wazalendo kilikuwa na masurufu yasiyorejeshwa yenye thamani ya Sh. 210,243,000 ambayo hayakuonyeshwa kwenye taarifa ya fedha ya Juni 30, 2015, hata hivyo.
MADUDU MENGINE
Katika ripoti hiyo, CAG pia anaeleza kuwa amebaini matumizi mabaya ya fedha za uwekezaji za Shirikisho la Serikali za Mitaa (ALAT) Sh. milioni 367.929.
Anasema ukaguzi umebaini ALAT ilipokea michango ya Sh. milioni 525.718 kutoka Mamlaka ya Serikali za Mitaa (LGA) kwa ajili ya mfuko wa uwekezaji, lakini mfuko uliokusudiwa haukuanzishwa na fedha zilitumika katika shughuli nyingine na menejimenti ya ALAT ilishindwa kutoa maelezo ya matumizi ya fedha hizo.
MFUKO WA RAIS
CAG anasema amebaini Mfuko wa Rais wa Uwezeshaji ulipewa mkopo wa kiasi cha Sh. milioni 514 chini ya Mpango wa Taifa wa Uwezeshaji Kiuchumi (NEEP) mwaka 2007/2008, fedha zake hazikutumika tena kama ilivyokusudiwa tangu 2009/2010; badala yake zilitumika kuwezesha shughuli za utawala kinyume cha madhumuni ya awali. Pia amebainika marejesho ya fedha hizo hayajafanywa kama ilivyokubaliwa.
TANZANSINO
Prof. Assad anasema ukaguzi wake wa 2015/16 umebaini Sh. milioni 773 zililipwa na SUMA JKT Makao Makuu ikiwa ni sehemu ya malipo ya Sh. bilioni 1.292 kwa ajili ya kununua hisa za Holley, katika uwekezaji usio na tija wa utengenezaji wa dawa na mambo yanayohusiana na dawa.
Anasema SUMA JKT iliingia makubalianao ya ubia wa pamoja na Kiwanda cha Holley na baadaye kununua kiwanda kutoka kwa Shanxi Provincial Technical Renovation and Equipment Corporation, ubia ambao uliitwa TANZANSINO ambapo mwaka 2007 umiliki wa hisa ulikuwa asilimia 55 kwa Holley na 45 kwa SUMA JKT.
"Nimebaini kuwa tangu kuanzishwa kwa ubia huo wa TANZANSINO mwaka 2007 mpaka muda wa kuitimisha biashara 2014, hakuna mapato yoyote yaliyopokelewa kulingana na umiliki wa hisa uliokubaliwa. Hivyo haikuwa busara kwa SUMA kununua uwekezaji usiokuwa na tija," anasema.
SHIRIKA LA MIZINGA
Prof. Assag anasema Shirika la Mzinga lilishindwa kutoa taarifa ya ununuzi na nyaraka za zabuni kwa ajili ya ununuzi wa boti ya usalama baharini kwa mkopo wa Euro 32,588,376 (Sh.79,352,695,560) hivyo hakuweza kuthibitisha mchakato wa ununuzi pamoja na mapato ya mkopo katika akaunti ya Escrow.
TANROADS
CAG Assad anasema kuwa katika ukaguzi wake wa 2015/16, ukaguzi wa mikataba ulibainisha kuwa TANROADS ina limbikizo la riba lililofikia Sh. bilioni 7.875 na dola za Marekani 714,066.08 kutokana na kuchelewesha malipo kwa wakandarasi ya Sh. bilioni 36.766 na dola 6,534,720.75.
Prof. Assad anasema mwaka 2015/2016, TANROADS haikulipa madai ya wakandarasi na washauri Sh. bilioni 20.271 na kwamba kushindwa kulipa madai katika mwaka husika huathiri vibaya mipango ya miaka unayofuata ambayo madeni hayo yatalipwa.
WAKALA WA MAJENGO
CAG anasema amebaini manunuzi ya bidhaa na huduma yaliyofanywa na Wakala wa Majengo (TBA) kwa Sh. milioni 178.718 kutoka kwa chanzo kimoja kinyume na utaratibu huku wakala huo ukinunuliwa vifaa vya ujenzi kwa Sh. milioni 74.139 kutoka kwa wauzaji ambao Muhtasari wa Ripoti Kuu ya Mwaka 2015/16 wa Serikali Kuu umebainisha hawakuwa wamekidhi viwango katika mazingira ambayo hayakuelezwa, hata hivyo.
"Nilibaini TBA ilipokea Sh. milioni 500 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (Idara ya Ujenzi) kwa ajili ya ujenzi wa Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam. Baadaye TTBA walihamisha Sh. milioni 500 kwenda kwa Meneja wa TBA Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa nyumba tano eneo la Bunju ambapo siyo lengo lililokusudiwa," anasema.
MFUKO WA MIRATHI
Katika ukaguzi wake, CAG Assad anasema amebaini fedha za mirathi ya kiasi cha Sh. milioni 169 zilitumika kwa matumizi yasiyohusiana na madhumuni ya mfuko wa mirathi.