Dkt. Bilali: kila mtu ni muathirika mtarajiwa wa ugonjwa Usonji



Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Mohammed  Gharib Bilal amewataka wadau mbalimbali kuwapa fursa watoto wenye usonji ili waweze kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zitakazo wafanya wasijione wapweke.

Makamu wa Rais  Mstaafu Dk. Bilal ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya usonji duniani iliyoandaliwa na taasisi ya 'KSIJ Central Board of Education' katika shule ya Al-Muntazir ambapo ameipongeza taasisi hiyo kwa kuanzisha kitengo maalum kinachotoa mafunzo kwa watoto wenye usonji na kufafanua kuwa siyo kazi rahisi kwani inahitaji rasilimali watu, wataalamu, fedha kuwa na moyo na uthubutu hivyo wadau na serikali kwa pamoja waunge mkono jitihada hizo na atafikisha kilio hicho kwa serikali ili kuunga mkono jinsi ya kuwasaidia watoto hao.
DK. Bilal ameongeza kuwa kila mtu ni muathirika mtarajiwa wa usonji kwani kila umri unavyozidi kwenda ndiyo kiungo kimoja baada ya kingine vinavyopoteza mawasiliano na hatimaye kupatwa na usonji hivyo ni vyema kujitoa kwa hali na mali  kuwafanya nao wawe ni  sehemu ya jamii, kwani malipo yake yanatoka kwa Mwenyezi Mungu.

DK. Bilal amechangia kiasi cha shilingi milioni moja huku akiahidi kuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan atachangia milioni 5 katika jitihada za kuwasaidia watu wenye usonji.
Kwa upande wake Bwana Imtiaz Lalji ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya KSIJ ameeleza kuwa jamii ndiyo inabidi iwe rafiki wa karibu wa watu hawa na kutimiza ndoto zao za kimaisha, huku akieleza kuwa kwa upande wao KSIJ wametoa ajira za wanafunzi watatu kwa watu wenye usonji kama walimu wasaidizi na kutoa wito  kwa serikali na sekta binafsi kutoa nafasi za ajira kwa watu wa namna hiyo.                        
Maadhimisho hayo ya siku ya usonji duniani yamebeba kauli mbiu isemayo "Tuwalinde na Tuwapende"
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items