RC Makonda ataja listi ya majina 13, ataka wajipeleke Polisi (+Picha 15)

Leo April 19, Umoja wa Wasanii wa Bongo Movie Kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Dar es salaam chini ya Paul Makonda Wamefanya maandamano ya amani kutoka Katika ofisi ya Mkuu ya Mkoa kuelekea Eneo la kariakoo, kwa lengo la  kufanya mkutano wa kuzuia Uingizwaji na Uuzwaji wa filamu kutoka Nje ya nchi kinyume cha utaratibu.

Mara baada ya kuwasili eneo la Kariakoo, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka wote wanaojihusisha na uuzaji wa CD za kutembeza mkononi pamoja na wanao-burn miziki ya wasanii kuacha vitendo hivyo kwani vipo kinyume  na sheria.

Akiongea katika maandamano ambayo yaliratibiwa na wasanii wa filamu na yeye kualikwa kama mkuu wa Mkoa alikuwa na matamko 7 amboyo yote yamelenga kukemea vitendo hivyo. Aidha ufumbuzi wa tukio hilo ama yoyote anayetaka kuuza filamu za nje inatakiwa wawe na vitambulisho maalumu.

Katika maagizo yote amewataja watu 13 ambao wanahitajika kujipeleka katika kituo cha kati cha Polisi Jijini humo siku ya ijumaa kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na matumizi ya mitambo ya kzalishia filamu. Pamoja na kuzuia filamu za ngono zisiingie mkoa wa Dar es salaam na wasipojipeleka atawafuta mwenyewe.

Amewataka wasanii kufurahia jasho lao kwani wanafanya kazi ya ziada katika kutekeleza kazi zao na kuanzia leo wasanii hao wataanza kunufaika nazo kwani sheria kali na utekelezaji utafuatwa.

Sakata ambalo linaumiza wasanii hao ni uuzaji wa filamu za nje ambazo gharama yake kuanzia 700 kwa bei ya jumla hadi 1000 rejareja.

Sheria ya filamu 1979 inamtaka muuzaji wa filamu za nje na ndani kufuta utaratibu maalum na akitaka kuingiza filamu yoyote lazima ajaze 'form' ya kuomba uingizaji huo.

Baadhi ya Wasanii waliohudhuria ni Wolper, JB, Kajala, Ray Kigosi, Richi Richi, Radio na Mafuvu.















Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items