WANANCHI mkoani Njombe wameleza
mashaka yao kwa mamalaka ya Mapato TRA wilaya ya
Njombe kutokana kutopewa lisiti za EFD wakati wa manunuzi ya huduma na bidhaa
mbali mbali katika eneo hilo.
Wananchi hao kwa nyakati
tofauti wakizungumza na Muungwana Blog wamedai kuwa wanapoulizia mashine hizo
hujibiwa na wafanya biashara hao kuwa ni hawazijui mashine hizo na hawana
majibu ambayo yalitafsiriwa na wananchi hao kuwa ni mipango ya ualaji kati ya TRA
na wafanyabiashara hao.
Mmoja wa wananchi hao ambaye hakutaka kutajwa
jina lake amesema kuwa alifika kwenye moja ya
Hoteli Mkoani humo na kuhudumiwa bila ya kupewa lisiti za malipo zinazotokana
na mfumo wa ulipaji kodi EFDs ambapo alilazimika kudai lisiti hiyo na kuambiwa
kuwa hakuna na kwamba wao hawajui uwepo wa mashine hizo.
Mwengine alituonyesha
ushahidi wa lisiti ambazo amerejeshewa baada ya kuhudumiwa ambazo sio za EFD.
“Nimeshangazwa kuona eti
wafanya biashara wa iringa wanadai kuwa hawana mashine za EFD na kwamba wanadai
kuwa hata watu TRA huwa wanakuja maenao hayo kupata huduma mbalimbali mfano
hapo Hotelini nilipokula naambia TRA hufika na kula hapo lakini hakuna mashine
za kukusanya mapato za EFDs.
![]() |
| lisiti zinazotumika kwenye Hotel mbalimbali katika eneo la Njombe |
Hata hivyo muungwana Blog
ilizungumza na Meneja wa TRA wilaya ya Njombe kuueleza mtandao huu kuwa yeye
hana Mamlaka ya kuzungumza na vyombo vya hanari hivyo tuzungumze na Meneja wa
Mkoa wa Iringa.
Muungwana Blog
ilizungumza na Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa Jeseph Kalinga , ambaye amesema kuwa kuhusu suala hilo anasikia kwetu
(mwandishi wa habari hizi) na kwamba ni vema watu wa eneo hilo wakaenda kwa Meneja
wa TRA wilaya ya Njombe na kueleza malalamiko hayo ili yafanyiwe kazi na kwamba
utakuwa ushahidi wa kuwawajibisha wafanya biashara wanaoepuka kutumia mashine
hizo.
Hata hivyo Kalinga
ameagiza wananchi kudai lisiti za EFD ili kuhakkisha kuwa wanalipa kodi kwa
ajili ya maendeleo ya taifa.
“Naomba hao watu waende
kwa Meneja TRA wilaya ya Njombe ili iwe rahisi kupata ushahidi wa wafanya
biashara gani wanaokwepa kutumia mashine hizo” amesema Kalinga.



