Msanii wa kizazi kipya kutoka nchini Uganda, Zaine Brown, yupo mtatani baada ya kuachia kibao kiitwacho Muyaye kinachomuongelea mchungaji wa kanisa anayewakamua waumini pesa.
Wimbo huo umekuwa na itikadi kali inayopinga tabia za wachungaji wanaotumia nyadhifa zao kuchuna pesa kwa washirika na wafuasi wao kwa kisingizio cha kuwaombea na kufanya miujiza ikiwemo kupata kazi na kadhalika.
Sasa baada ya kibao hicho kutoka, mchungaji mmoja wa Kampala ambaye ni maarufu, amenukuliwa akisema anampa siku nane Zanie kuomba msamaha kwa kumkejeli yeye pia na wachungaji wengine nchini Uganda, lasivyo atakiona kilichomfanya kanga kukosa manyoya ya shingo.
Kumekuwa na mijadala kuhusiana na suala hilo, lakini Zanie amelikaushia na hajaweka wazi iwapo yupo tayari kuomba msamaha ama hatojali vitisho vya mchungaji huyo ambaye anafahamika kama Pastor Kakande.
Hata hivyo mashabiki wengi wa muziki wa kizazi kipya nchini humo, wamemuunga mkono staa huyo na kumdhihaki Mchungaji Kakande ambaye wengi wamesema anajishuku kuwa huenda kaimbiwa yeye wimbo huo ambao hata jina lake halikutajwa ndani kwenye mashairi ya wimbo huo.
Chini hapa nimekusogezea kibao chenyewe kwa jina Muyaye.