Arsene Wenger amfuata Mbappe hadi nyumbani

London, England. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kwamba amepiga hatua kutokana na kwenda kumtembelea Kylian Mbappe nyumbani kwake ikiwa ni njia ya kumshawishi ajiunge na klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo wa Monaco amekuwa akihusishawa kujiunga na klabu mbalimbali barani Ulaya baada ya kupata mafanikio makubwa msimu huu akiwa amefunga mabao 24 kwenye mechi 39 alizocheza katika mashindano yote.

Jeuri ya Wenger inatokana na maelezo yake kwamba wana uhisiano mzuri na klabu ya Monaco hata uhamisho wa mchezaji huyo ni jambo lahisi iwapo watafikia mwafaka, huku akisema kwamba hata Thiery Herny alitoka huko.
Mpya zaidi Nzee zaidi