Waziri auawa kwa kushambuliwa na risasi Somalia

Waziri wa kazi za umma na ujenzi  Abbas Siraj amepigwa risasi na kuuawa baada ya vikosi vya serikali kummiminia risasi wakati akaiwa kwenye gari lake mjini Mogadishu nchini  Somalia.

Kwa mujibu wa habari,mashambulizi hayo yamefanywa mbele ya ikulu ya rais,wakati waziri huyo akitoka katika shughuli zake.

Mkuu wa polisi wa eneo hilo amesema kuwa waziri aliyeuawa alishambuliwa na vikosi hivyo vya serikali wakati yumo ndani ya gari lake katika wilaya ya Warta Nabada.

Abbas Siraj,mwenye umri wa miaka 31 ndiye alikuwa waziri mdogo kuliko wote serikalini.

Siraj alikulia Dadab,kambi kubwa ya wakimbizi nchini Kenya .

Siraj alichaguliwa kwa kura za ndio katika jimbo la Jubaland nchini Somalia.

Waliohusika na shambulizi hilo kuchukuliwa hatua.
Mpya zaidi Nzee zaidi