Zanzibar. Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM Zanzibar, Waride Bakari Jabu amewataka wanachama wa chama hicho tawi la Chukwani kutumia vizuri fursa ya uchaguzi kuwachagua viongozi na watendaji waadilifu na wasioyumbishwa wanapotekeleza majukumu yao.
Akizungumza na wanachama na kamati ya siasa ya tawi hilo alisema safu za viongozi wa ngazi mbalimbali watakaochaguliwa kupitia uchaguzi ndani ya chama hicho ndiyo watakaokuwa na jukumu la kuwaidhinisha viongozi watakaoivusha CCM salama na kuhakikisha inashinda katika uchaguzi mkuu ujao.
Aliwaagiza viongozi wa ngazi ya majimbo ambao ni mbunge, mwakilishi na madiwani kuhakikisha wanawapatia wananchi taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 ili wajue ahadi zilizotekelezwa na kuhoji ambazo bado utekelezaji wake.
“ Viongozi lazima tuendeleze utamaduni wa kuwa karibu na wananchi kwa kuwa ndio waliotuajiri katika nafasi hizi tulizonazo na mkataba wetu na wao ni kuwatatulia kero zinazowakabili katika maeneo yao,” alisema.