Chadema: Bunge la July kuwaka moto

Dar as Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema bunge litakaloanza July mwaka huu litawaka moto kwa sababu ya matukio yanayoendelea na jinsi serikali inavyoendesha nchi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo, Mnyika alisema  hata wabunge wa CCM nao wataonyesha wazi kuchoshwa na mambo yanayoendelea ikiwamo vyombo vya usalama kutumia silaha hadharani.

Akifafanua kuhusu maamuzi ya mkutano Mkuu wa chama uliomalizika hivi karibuni alisema umekubaliana kwa kauli moja kuwapitisha Ezekiel Wenje na Lawrence Masha kuwania uwakilishi wa chama kwenye bunge la Afrika Mashariki.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items