Msimu wake wa kwanza tu Uingereza ameipa Chelsea ubingwa wa nchini humo, huku likiwa kombe lake la nne ndani ya misimu minne mfululizo kama kocha.
Baada ya kuipa Chelsea ubingwa huo Conte alizungumza na waandishi wa habari, moja kati ya vitu vikubwa kusema ni ugumu alioupata alipojiunga na ligi ya Uingereza na jinsi ilivyokuwa kazi kwao kubeba ubingwa.
“Haikuwa rahisi kwangu kufanya hiki, kwani nilikuja hapa huku lugha inanisumbua na kukutana na wachezaji wengi wapya huku wakiwa wametoka kwenye msimamo ambao haukuwa mzuri”
Conte anaendelea kusema kwamba ubingwa huo wa Chelsea msimu huu ni maalum kwa ajili ya wachezaji wake wote kwani anaamini walijitoa sana kwa ajili ya ubingwa huo.
“Walionesha kuwa na hamu ya kutaka kufanya jambo kubwa sana na sasa naamini watakuwa nafuraha na msimu umetutendea haki, wakati tunaanza hatukuwa vizuri lakini sasa kikosi kimeimarika” alisema Conte.
Conte anaamini mfumo wake wa 3-4-3 ndio umechangia kwa kiasi kikubwa Chelsea kubeba ubingwa lakini akasema vijana wake wamepambana sana na ndio maana ubingwa huo ni wa kwao.