Roma Mkatoliki Amjibu Mbunge Kessy, adai aliongea uongo mtupu



Katika kipindi cha Clouds360 kinachrushwa na Televisheni ya Clouds media, msanii RomaMkatoliki ameonyesha kukasirishwa na kitendo cha Mh Kessy ( Mbunge wa Jimbo la Nkasi ) kutaja jina lake Bungeni na kudai kwamba Roma aliimba wimbo kumhusu Rais. Hivi karibuni Mh Kessy aliongelea ' sakata la kutekwa kwa Roma ' na kudai kwamba hayo yalitokea baada ya Roma kuimba wimbo unaomkashifu Rais.

RomaMkatoliki ameeleza kwamba alisikitishwa na kitendo hicho kwani Mbunge huyo alichokisema kilikuwa kitu cha uongo. " Tena alitaha kabisa jina langu. Akitoka nje ya Bunge yule ukimuuliza hana uhakika. Lakini ameongea vile kwa sababu yeye ana mahali pa kusemea. Je mimi mimi nitasemea wapi ? " - Roma Mkatoliki
.
.
Roma alimaliza kwa kusema kwamba yeye kazi yake ni muziki hivyo anashangaa mwanasiasa kuzungumza maneno hayo " Hayo maneno bora angeongea  RaisWaManzese ( @madeeali ) ningejua swahiba wangu ananitania . " akimaanisha Madee
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items