Wananchi walalamikia daraja lililojengwa chini ya kiwango Dar

Daraja linalounganisha Bangulo na Pugu Mzimbazi limeharibika tutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha  jijini Dar es salam.

Wananchi wamelalamika kuwa Daraja hilo  lilikabidhiwa Mwaka jana na manispaa ya Ilala Baada ya Kukamilika ujenzi wake ambao ulikuwa chini ya Mkandarasi wa Manispaa ya ilala.

Hata hivyo Uchunguzi unaonyesha Kuwa Daraja Hilo lilijengwa Chini ya Kiwango Nondo zilizo tumika hapo ni (mm 12) ambazo hutumika kujengea nyumbani za kawaida.









Wananchi walikabidhiwa daraja hilo na Manispaa ya ilala kutoka kwa makandalasi wa Manspaa hiyo.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Saidi Mpili amesema kuwa daraja hilo lilijengwa chini ya kiwango ingawa serikali ya mtaa ilishindwa kushauri kutokana na ujenzi huo kusimamiwa na Manspaa (Ilala)

Ofisa Mtendaji wa kata ya Victor Shekimweli amezungumza na Muungwana Blog kwa njia ya simu amethibitisha kuhalibika kwa daraja hilo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.

Shekimweli amesema kuwa Mkandalasi wa daraja hilo hakuzingatia kuwa eneo la mto huo (Msimbazi) hujaa maji na kusababisha kumong’onyoa kingo za mto huo.

Diwani wa Kata ya Pugu Station Yohana Ng'ong'a naye amesema kuwa tayari maeripoti ubovu wa daraja hilo kwenye kikao cha Manspaa na kwamba daraja hilo lipo chini ya kiwango kulinganisha na gari zinazopita hapo ambapo daraja hilo haliwezi kuhimili vishiondo vizito.

Ng'ong'a ameeleza kuwa daraja hilo linapitisha maroli yanayobeba ng'ombe kupeleka mnada wa Pugu yenye zaidi ya tani 18.

Meya wa Manspaa ya Ilala Charles Kuyeko, aliiambia Muungwana kuwa atafika kwenye eneo hilo hivi karibuni akiwa na Mhandisi pamoja na Mkandarasi kwa ajili ya majibu kuhusu ujenzi wa daraja hilo na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wahusika.

Amesema mwaka jana   Manspaa hiyo iliwachukulia hatua wakandarasi wa Manspaa hiyo waliojenga miundombinu chini ya kiwango.


.




Mpya zaidi Nzee zaidi