WANAWAKE wawili ni miongoni mwa watu sita waliotiwa mbaroni na Jeshi la Polisi mkoa wa Geita kwa tuhuma za kuwaua watu watatu, mmoja wao akichomwa moto, na wa nne kuokolewa na polisi, wakituhumiwa kuiba debe 16 za mahindi katika mtaa wa Mwatulole, kata ya Buhalahala wilaya na mkoa wa Geita katikati
Akithibitisha jana kukamatwa kwa watuhumiwa sita hao, Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Lodosn Mponjoli alisema watuhumiwa hao wanahojiwa ili kusaidia polisi upelelezi wake na watakaoabinika walikua chanzo cha mauji hayo watafikishwa mahakamani.
Watu hao waliuawa Alhamisi saa tatu asubuhi kwa tuhuma za kuvunja usiku chumba kulimokuwa kumehifadhiwa debe 16 za mahindi.
Kamanda Mponjoli alisema mmoja wa marehemu hao anadaiwa kupatikana akiuza mahindi na baada ya kukamatwa, aliwataja wenzake.
Baada ya kupekuliwa vyumbani mwao, moja ya chumba kulikutwa mali zinazodhaniwa kuwa za wizi na kutambuliwa na wenyewe hatua iliyowapandisha hasira wananchi na kuanza kuwashambulia kwa kipigo, alisema kamanda huyo.
Wanaodaiwa kuuawa kwa kupigwa kwa mawe na fimbo wametambuliwa kuwa ni Mwana Athuman (45), Linze Richard (39) na aliyejulikana kwa jina moja la John.
Mtuhumiwa wa nne, Matokeo Malomo (20) mkazi wa kijiji cha Mpomvu, kata ya Mtakuja wilayani Geita aliokolewa na polisi na alipohojiwa anadaiwa kukiri kushirikiana na marehemu hao kuiba mahindi.
Kamanda Mponjoli aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Mathais William (36), Richard Kiteu (51), Patrick Edward (42), Daud Andrea (49), Merisiana Jospeh (39) na Mariam Zakayo (27).
Mkuu huyo wa Plisi alikemea vitendo vya kujichukulia sheria mikononi akisema kamwe havitovumiliwa kwani vinajenga chuki na visasi katika jamii.
Kumekuwapo kwa uhaba na bei ghali ya chakula katika maeneo mengi ya nchi, mkoa wa Geita ukiwa mmojawapo.
Uchunguzi wa Nipashe unaonyesha hali hiyo imetokana na ukame wa muda mrefu ambao ulisababisha mazao kukauka.
Gunia moja la mahindi (sawa na debe sita) linauzwa kwa bei ya wastani wa Sh. 112,000 kwa sasa, uchunguzi wa Nipashe umeonyesha.
SH. 65,000
Matukio ya watu kuuawa na kisha kuchomwa moto mkoani Geita yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara tangu wanaume watano kuuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kuchomwa moto kwa tuhuma ya kuiba Sh. 65,000 za rambi rambi Desemba 2013.
Marehemu hao walishambuliwa wakiwa mikononi mwa walinzi wa jadi (sungusungu).
Watu hao walidaiwa kuiba mchango usiku nyumbani kwa John Ibarabara baada ya kuvamia nyumba ya mfiwa ikiwa ni siku moja baada ya ndugu, marafiki na majirani, wakiwemo watuhumiwa kutawanyika.
Ilidaiwa kuwa marehemu hao walirudi nyumbani kwa mfiwa usiku na kuvunja mlango na kutaka wapatiwe fedha ya rambirambi, walifanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa akiwa na damu kwenye nguo zake na walipomhoji aliwataja watu wengine ambao walikamatwa wote.