Maswali Magumu kwenye Kesi ya Ukuta Lissu Vs Serikali.


Kesi ya Ukuta inayomkabili Juma Mtatuu imeendelea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jana ambapo Upande wa Utetezi unaowakilishwa na Lissu waliwasilisha hoja ya kutaka kuondolewa kwa Mashtaka hayo kutokana na Udahifu wa Hati ya Mashtaka.
Matatuu anadaiwa Kuandika Kwenye mtandao wake Facebook taarifa za kuridhihaki jeshi la Polisi ambapo Tarehe 24 Agosti Mwaka 2016 kwa kuandika maneno haya; “huyu hata akifa ataenda peponi na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala. Mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama. Tarehe 1 Naelekea Kahama kwa Ukuta mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta. Kifo kipo tu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha?”


Wakili Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendele Chadema Tundu Lissu amewasiliasha Hoja mbili Mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa kuwa Mahakamia hiyo itupilie mbali kesi hiyo kutokana na Hati ya Mashatka kuwa Mbuvu.
Lissu amedai kuwa hati hiyo haijitoshelezi kumwezesha Mshtakiwa kupeleka utetezi wake mahakamani hapo kutokana na maelezo yake kuwa hayajitosheleza.

Hoja za Lissu; kwenye hati ya mashtaka kumelezwa huyu hata akifa ataenda peponi, Huyu ni nani?,
Lissu; Kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala, Kina nani?  Mbagala gani?.
Mimi nitakuwa wa Kwanza kuandamana kule kahama , mandamano ya namna gani? ilhali maandamano ni halali kwa mujibu wa sheria.
Mimi nitakuwa wa kwanza kushika bendera ya Ukuta , Bendera ya Ukuta ni ipi?
Lissu; Tarehe 1 Naelekea Kahama kwa Ukuta, Tarehe Moja ya Mwezi gani na inamaanisha nini? Ukuta nini?

Hoja nyengine ya Lissu ni Kuhusu kesi ya Kudhalilisha Jeshi la Polisi ambapo alidai kuwa ni Sharti kuwepo kwa mtu au nafsi iliyokasirishwa , kuumizwa na na hiyo kauli iliyomdharirisha, “kwenye hati ya Mashtaka kuna jeshi la Polisi ambalo sio mtu.”
Lissu alidai kuwa hati ya Mashtaka ingeeleza ni nani hasaa aliyeumizwa kama ni IGP, au Kamshna Fulani lakini hakuna mtu aliyetajwa kwa na kwamba aliomba Mahakama itupilie mbali keshi hiyo.

Kwa Upande wa Wakili Mwandamizi wa Serikali Kishenyi Mutywalemwa amedai kuwa dawa ya Hati Mbovu ya Mashtaka sio kuondo kesi ni kuleta nyengine “ lakini maelezo ya hii hati ya mashtaka ipo wazi kulingana na Muktadha wa muda’
Mutalemwa alidai kuwa ushahidi upo na utafikishwa mahakamani kuthibitisha lakini pia Tarehe 24 Agosti 2016 inajiieleza na Maana ya Ukutu huwezi kuiweka kwenye hati ya mashtaka.
Mutalemwa amedai kuwa Jeshi la Polisi linaundwa na watu na ndio waliodharishwa .
Hakimu Mwamba amesema kuwa Maamuzi ya kesi hiyo yatatolewa tarehe 6 Juni mwaka huu.



Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items