Serikali yafuta posho za madiwani Dar

Meya wa Dar es salaam Isaya Mwita

 Leo Julai 1 2017, Baraza la Madiwani Jijini Dar es salaam limekaa kikao cha kawaida kujadili ripoti yake ya mwezi januari- Machi yenye agenda  kadhaa ikiwemo Agenda ya kusomewa taarifa kutoka TAMISEMI kuhusu kusitisha fedha za kuchochea maendeleo kuingia kwenye akaunti za madiwani ,ambapo kwa kauli moja madiwani wote wametamka kutoielewa na kumuagiza Mkurugenzi wa Jiji kuomba ufafanuzi kutoka TAMISEMI ili waweze kuijadili vizuri. 

Taarifa hiyo iliyosomwa na Afisa utumishi wa Jiji Waziri Kombo kwaniaba ya Katibu mkuu TAMISEMI mbele ya mstahiki meya Isaya Mwita imetamka kuwa Kwasasa fedha zote za maendeleo ya kata zitapelekwa moja kwa moja kwenye Akaunti ya Kata badala ya Akaunti ya Diwani, ambapo baadhi ya madiwani wameshangaa na kusema fedha hizo hazijawahi kuingizwa kwenye akaunti zao na kwamba Serikali itakua imepotoshwa, na kwamba kufanya hivyo ni kuwafanya madiwani washindwe kutkelewa majukumu yao.
Waziri Kombo

Baadhi ya Madiwani kutoka Upinzani wamefika mbali zaidi na kusema kuwa ni njama za serikali kuudhoofisha upinzani ili washindwe kufanya maendeleo kwenye kata zao, kwakuwa kwasasa Halmashauri za jiji hilo kwa idadi kubwa zipo chini ya Wapinzani.
Patrick John Asenga (Diwani CHADEMA)

Hata hiovyo kwa Upande wake mstahiki meya Isaya Mwita amesema Haoni kama ni Jambo baya ingawa amekiri kuwa fedha hizo zilizoondolewa zilikuwa zikiwasaidia sana madiwani katika kuhamasisha maendeleo, kwahivo kwakuwa ndio limeanza kujadiliwa anaamini litakaa sawa.
Mpya zaidi Nzee zaidi