F lori laua mtu mmoja Songea | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

lori laua mtu mmoja Songea

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la SULTAN YUSUPH, ambaye alikuwa utingo, mkazi wa Kibaha Mkoani Pwani,amefariki dunia baada ya lori aina ya Howo kupinduka katika Kijiji cha Gumbiro Wilaya ya Songea Mkoani  Ruvuma.

Lori hilo  lililokuwa limebeba makaa ya mawe lilikuwa likitokea Kitai Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma, GEMINI MUSHY amesema kuwa dereva wa  lori  hilo amejulikana kwa jina la KAZI YUSUPH na kwamba gari hilo ni mali ya kampuni ya Sun Shine ya Wilayani kibaha mkoa wa pwani na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari hilo kuendesha gari kwa mwendo kasi.

Kamanda MUSHY amesema hali ya dereva wa gari hilo inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kutokana na majeraha aliyoyapata katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Ametoa wito kwa madereva kwamba jeshi hilo litaongeza kasi ya kuwapima kiwango cha ulevi madereva wote ili kuondokana na ajali zinazo sababisha kupoteza maisha ya Watanzania.