F Mwingine ajiuzuru kwenye uongozi wa Trump | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mwingine ajiuzuru kwenye uongozi wa Trump

Mwanachama wa kamati ya washauri wa kidini ya Donald Trump ametangaza kujiuzulu siku ya Ijumaa kufuatia kauli ya rais huyo katika mkutano wa watu weupe pekee.

A.R. Bernard ambaye ni kiongozi wa wafuasi  37,000 wab chama cha Utamaduni wa Kikristo aliambia CNN kwamba amejiondoa kabisa kutoka bodi hiyo .

Bernard ni raia wa Marekani mwenye asili ya kiafrika ambaye pia ni mwanachama wa bodi ya wanachama 25 wa kidini katika White House .

Baada ya kuwa na ghasia zilizosababishwa na ubaguzi wa rangi rais Trump alisema wazi wazi kwamba makundi yaliyohusika yote yalisababisha vurugu hizo haatari jambo ambalo lilizua ukosoaaji mkuu kutoka kwa Republicans na Democrats .