Wachezaji wa England wakishangilia ubingwa wa Kombe la Dunia la Vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya ushindi wa 5-2 dhidi ya Hispania leo mjini Kolkata, India. Mabao ya England yalifungwa na Rhian Brewster, Morgan Gibbs White, Phil Foden mawili na Marc Guehi, wakati ya Hispania yalifungwa na Sergio Gomez.
