Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Visiwani Zanzibar Mh Ayoub Mahmoud amewashukuru waandishi wa habari kwa kufanya uhamasishaji wa wananchi
kujitokeza kwa wingi katika kilele cha mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na
kumbukizi za miaka 18 kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
RC
Ayoub amewashukuru vioongozi wote wa kitaifa walioandika historia kwa
kuhudhuria kilele hicho cha mbio za Mwenge katika uwanja Amaan visiwani humo.
RC
Ayoub amewapongeza wnanchi wote waliojitokeza kwani wametoa hamasa
kubwa jambo lililopelekea mgeni rasmi wa shughuli hiyo Rais John Pombe
Magufuli kupongeza maandilizi yaliyofanywa kwa ustadi wake na
kifanikisha tukio kuhitimishwa salama.
RC
Ayoub amewaomba wanahabari na wananchi kuendelea kushirikiana na
serikali kwa maendeleo ya taifa, pia ameyashukuru makampuni mbalimbali
kwa kujitolea kufanikisha kilele cha mbio za Mwenge na huduma mbalimbali
za kijamii.
