Wakili wa kujitegemea Jebra Kambole amezungumza na Muungwana Blog na kusema kuwa, Kwa mujibu wa kifungu namba 195, sura ya 16 kanuni za adhabu ndio kifungu kilichoelezea maana ya kesi ya kuua bila kukusudia na adhabu zake.
Katika sheria ya kuua bila kukusudia (manslaughter) kunatofautishwa na kuua kwa kukusudia (murder) kwenye kifungu hicho. Kuua bila kukusudia ni kuua ambako muuaji anatenda kitendo hicho kinachopelekea umauti lakini bila dhamira, lengo au nia ya kukusudia kuua.
Wakati kuua kwa kukusudia ni pale mtu anapotenda tendo ambalo linapelekea mauaji ya mtu lakini amefanya hivyo akiwa amedhamiria kuua. Kwahiyo haraka utaona kuwa tofauti kubwa ya kuua kwa kukusudia na ile ya kuua bila kukusudia ni dhamira, nia au lengo.
Je, utajuaje kuwa mtuhumiwa aliua bila kukusudia na zipi adhabu zake?
TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI
