Mshambuliaji wa Brazil ahukumiwa kwenda jela


Mchezaji soka wa Brazil Robinho amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela kwa kushiriki katika genge lililombaka mwanamke mmoja mjini Milan mwaka 2013.

Mahakma ya Italia imesema kuwa Robinho mwenye umri wa miaka 33- na raia wengine wa Brazil walimbaka mwanamke raia wa Albania , aliekuwa na umri wa miaka 22, baada ya kumnwesha pombe kwenye kilabu cha usiku mjini Milan.

Mchezaji huyo wa safu ya ushambuliaji, aliyeondoka katika klabu ya AC Milan mnamo mwaka 2015 baada ya kuichezea miaka mitano hakuwepo mahakamani wakati wa hukumu hiyo lakini alikana mashataka dhidi yake kupitia wakili wake.


  • Pirlo atangaza kustaafu soka


Hukumu hiyo haitatolewa hadi pale mchakato wa rufaa utakapokamilika.

Robinho, aliichezea Manchester City na sasa anachezea timu ya Atletico Mineiro nchini Brazil.


  • Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 23.10.2017


Ujumbe kwenye ukurasa wa Instagram wa Robinho unasema "tayari amekwisha jitetea dhidi ya shutuma, akisisitiza kuwa hakushiriki katika tukio hilo " na kwamba "hatua zote za kisheria zinachukuliwa".


  • Brazil vinara wa soka Ulimwenguni


Baada ya kuanza taaluma katika Santos, Robinho alishinda mataji mawili ya La Liga katika kipindi cha misimu minne katika Real Madrid, kabla ya kujiunga na City kwa malipo ya Euro milioni 32.5 (£32.5) wakati wa msimu wa kiangazi mwaka 2008.

Hata hivyo Robinho alikabiliwa na kibarua kigumu cha kuonyesha uwezo wake wa ziada katika soka ya England ndipo alipolazimika kurejea Santos Januari 2010.