TPRI wakamata viuatilifu vilivyoisha mda wake Mbeya

Taasisi ya utafiti wa viuatilifu nchini,TPRI,imekamata shehena ya viuatilifu ambavyo muda wake wa matumizi umepita na vingine vikiwa havijasajiliwa nchini vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisa vikiuzwa katika maduka ya viuatilifu jijini Mbeya.

Wakaguzi kutoka taasisi ya utafiti wa viuatilifu nchini, TPRI, wameifanya ukaguzi kwenye baadhi ya maduka ya viuatilifu katika maeneo ya Uyole jijini Mbeya ambako wamekamata shehena ya viuatilifu ambavyo muda wake wa matumizi umepita na vingine vikiwa havijasajiliwa nchini huku baadhi ya wafanyabiashara wakikutwa  wamebadilisha vifungashio vya baadhi ya viuatilifu kwa kuvimimina kwenye chupa za pombe na kuwauzia wananchi jambo ambalo wakaguzi hao wamedai ni kinyume na sheria ya uuzaji wa viuatilifu.

Baadhi ya wauzaji wa viuatilifu wamedai kuwa idadi kubwa ya wateja wao hawana uwezo wa kiuchumi kununua chupa nzima za viuatilifu kama zilivyotoka kiwandani na ndio sababu huamua kuvimimina kwenye chupa zenye ujazo mdogo ili kila mwenye mahitaji aweze kumudu kununua.

Shehena ya viuatilifu vilivyokamatwa vitateketezwa kwa kuzingatia sheria za nchi ili kwa lengo la kudhibiti ubora wa viuatilifu vinavyotumika nchini