Mimi Mars akana kutoka kimapenzi na Joh Makini

Diva kutoka kiwanda cha Bongo Fleva Mimi Mars amekisanua kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Rapa kutoka kampuni ya Weusi Joh Makini na kinachoongelewa dhidi yao ni stori ambazo hazina ukweli wowote.

Akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, Mimi Mars amesema yeye na Joh Makini ni sawa na mtu na kaka yake, kwani Joh Makini alikuwa rafiki kipenzi wa kaka yake.

“Mahusiano yangu mimi na Joh Makini ni ya kidada na kaka, kwa sababu Joh Makini ni mtu ambaye tumemjua kuanzia tukiwa wadogo, alikuwa rafiki yake kaka yangu mkubwa, kwa hiyo kama ambavyo kaka yetu mkubwa anatushauri ni sawa na Joh Makini, ni rafiki, ni kaka, ni mshauri, sijui suala la mahusiano limetoka wapi”, amesema Mimi Mars.

Mimi Mars amesema kwa sasa hayupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote akikusuia kufocus kwenye kazi zake zaidi.

EATV.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items