Wazazi na walezi wenye nia ya kuwasomesha watoto wao China wameshauriwa kutumia njia sahihi za kuwasiliana na vyuo ikiwemo ubalozi wa nchi yao ili kulipa ada moja kwa moja kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi wanapokelewa bila utapeli.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Soma China Consulting and Service Co.Limited, Ru Lin amesema hayo jijini hapa kuwa baadhi ya wazazi na walezi wamejikuta wakitumia fedha nyingi kwaajili ya kupeleka watoto China wakati wanaweza kutumia gharama nafuu na kuwawezesha watoto wao kupata elimu bora.
Amesema kutokana na changamoto hiyo kampuni hiyo imeandaa maonyesho ya vyuo vikuu tisa vinavyotoa elimu katika sekta mbalimbali yatakayofanyika Shule ya Sekondari Arusha kwa siku tatu ambayo yatafunguliwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha,Richard Kwitega .
“Baadhi ya Watanzania wamekua wakipata changamoto ya kutumia fedha nyingi kwaajili ya kupata wakala wa kumwezesha kupata vyuo vizuri wanavyotaka lakini ni vyema wanatumia Ubalozi wetu hapa nchini kwaajili ya kujua aina za vyuo vikuu vilivyopo China na kiwango cha ada ili kuepuka udanganyifu,”amesema Ru
Amesema licha ya nchi yao kupiga hatua kubwa kimaendeleo wanahimiza nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania kutumia njia sahihi za kupata vyuo vinavyotoa elimu nzuri ambayo itawasaidia wahitimu baadaye na kuwataka kuhudhuria maonesho hayo.
Kwa upande wake ,Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Arusha, Christopher Malamsha amewataka wazazi na walezi kufika kwenye maonesho hayo ili kufungua fursa za elimu kwa watoto wao badala ya kutumia gharama kubwa kutafuta vyuo kwa njia zisizo rasmi.
Amesema kuwa elimu ni msingi bora katika maisha ya kila mwanadamu hivyo elimu bora inatokana na mzazi alivyowekeza kwa mtoto wake na kuwa maonyesho hayo ya vyuo vikuu tisa kutoka China yatatoa fursa ya kujifunza.