Uwanja wa Uhuru noma, watumika na Timu tatu

Ule msemo wa Uhuru ni Shamba la bibi, ulikuwa ni msemo sawa baada uwanja huo kuwa kimbilio la timu nyingi kufanya mazoezi uwanjani hapo.

Leo asubuhi uwanja huu, ulitumika na vilabu vitatu, huku vilabu viwili vikiwa kutoka ligi Daraja la kwanza ambavyo vinapigania kupanda daraja.

Majira ya Saa moja asubuhi KMC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ndio iliyoanza kuutumia uwanja huu mpaka majira ya saa mbili na dakika kumi na tano, kisha Africa Lyon kuutumia uwanja huo saa mbili na nusu mpaka saa tatu na nusu kisha kuwapisha Yanga.

Lyon inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 21 katika kundi A, kesho watashuka Dimbani kucheza na Ashanti United, huku Friends Rangers inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 22 wao watakipiga JKT Ruvu kutafuta tiketi ya kupanda Ligi Kuu
Mpya zaidi Nzee zaidi