Wajisaidia kwenye chanzo cha maji kukomesha wenzao

Mgogoro wa kugombea mradi wa maji kati ya kata ya Fulwe na Bamba mkoani Morogoro umeingia katika sura mpya baada ya wananchi wa kata ya Bamba kuingia kwenye chanzo cha maji cha Bamba na kuanza kuogelea, kukojoa ili kuwakomesha wananchi wa kata ya Fulwe.

Akizungumzia mgogoro hupo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Morogoro, Sudi Mpili alisema mwezi uliopita wananchi wa kata ya Bamba walipasua miundombiu ya maji inayokwenda Fulwe ingawa baadaye ilitengenezwa.

Alisema sababu kuwa iliyopelekea mgogoro huo kiasi cha wananchi wa kata ya Bamba kufanya uharibifu huo ni kitendo cha miradi yao kuchelewa kukamilika.

Mpili alisema kwamba tayari wameshatoa taarifa kituo cha Polisi ili kuweza kusaidia kukomesha vitendo hivyo na kuwataka wananchi wa Bamba kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kusaidia kuwapata kikundi hicho cha kihuni.

" Nishafanya mikutano mingi na wananchi wa Bamba na kuwataka wawe watulivu kwani mradi wa maji siyo wa eneo fulani ni wa kila mtu, lakini kuna kikundi cha wahuni ambacho kimekuwa kikifanya uharibifu huu, niseme tu tushawasiliana na Jeshi la Polisi ili waweze kuwatia mbaroni," alisema Mpili.
Mpya zaidi Nzee zaidi