Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imewahamisha madaktari wake bingwa 15 na wauguzi 30 kwenda katika Hospitali ya taaluma na Tiba ya Mloganzila ili kuongeza nguvu ya huduma kama ile inayotolewa Muhimbili.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepongeza hatua hiyo iliyochukuliwa huku akisema itaongeza ari na nguvu ya kufanya kazi kwenye Hospitali hiyo.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo alipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kujionea utoaji huduma lakini pia kukagua maendeleo na agizo lake alilolitoa la kutaka baadhi ya wagonjwa kuhamishiwa Hospitali ya Mloganzila.
" Niliwaagiza MNH kuhamisha wagonjwa waliopo kwenye jengo la Mwaisela kuanzia wodi namba 3,4,5,6,7 na 8 isipokuwa wale ambao ni wagonjwa mahutihuti, nawapongeza kwa kutekeleza agizo hilo," Alisema Ummy.