Wizara ya Kilimo kupitia Idara ya Udhibiti wa Mbolea(TFRA) imetumia magari ya jeshi kupeleka mbolea kwenye mikoa yenye upungufu ukiwemo Mkoa wa Rukwa.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Rais John Magufuli kuutaja Mkoa wa Rukwa kukosa mbolea alipokuwa akizunguza jana Ikulu Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa TFRA, Lazaro Kitandu aliyekuwa akisimamia upakiaji wa mbolea hiyo katika ghala la kampuni ya Premium lililopo Vingunguti Dar es Salaam leo Jumanne amesema magari saba ya jeshi yamepeleka tani 500 Rukwa leo, ili kuitikia wito wa Rais Magufuli.