Rais Joao Lourenco amelihakikishia taifa kuwa uhusiano wake na mtangulizi wake Jose Eduardo Dos Santos ni “mzuri” licha ya marekebisho ya kiuchumi yanayoonekana kuilenga familia ya mkuu huyo wa nchi wa zamani na washirika wake.
“Sioni mgongano wowote katika uhusiano wetu,” Lourenço aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu. “Rais wa chama anaongozwa na katiba ya chama, na kama Rais wa Jamhuri naheshimu na kutii Katiba,” aliongeza.
Kuhusu uchumi, Lourenco alisema kwamba uchumi hauwezi kurekebika bila kuchukua hatua kali na akafuta uwezekano wa nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi “kwa sasa”.
“Uchumi ukiwa bora kiasi, itakuwa haki kuongeza mshahara lakini siyo kwa sasa,” alisema Lourenco.
Baada ya kula kiapo cha kuiongoza Angola na kuanza kutekeleza ilani yake Lourenco haraka aliwafuta kazi maofisa 60 wa serikali akiwemo mwanamama mwenye nguvu Isabel Dos Santos ambaye alikuwa akiongoza kampuni ya taifa ya mafuta ya Sonagol.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Lourenco aliashiria kwamba mabadiliko mengine yanakuja katika usimamizi wa mfuko wa fedha wa taifa.
Mfuko huo wenye dola za Marekani 5 bilioni unasimamiwa na mtoto mwingine wa mtangulizi wake Jose Filomeno dos Santos. Lourenco amesema anafikiria kubadili uongozi lakini itategemea ripoti ya ukaguzi wa nje unaofanywa juu ya utendaji wake na usimamizi ambao unatarajiwa kukamilishwa hivi karibuni.
0