TIMU ya Arsenal inaweza kumkosa mshambuliaji wake, Alexandre Lacazette kwa wiki sita baada ya Mfaransa huyo kufanyiwa upasuaji wa goti lake la mguu wa kushoto.
Klabu imethibitisha Lacazette aliumia goti na kufanyiwa upasuaji jana asubuhi na atakuwa nje kwa wiki sita baada ya zoezi hilo.
Arsenal imesema upasuaji wa goti hilo umetokana na tatizo dogo, lakini Lacazette atapatiwa tiba zaidi.
Lacazette alipoteza nafasi mbili nzuri za kusawazisha Jumamosi Arsenal ikifungwa 1-0 na mahasimu wao wa London, Tottenham baada ya kuingia akitokea benchi.
Mfaransa huyo alijiunga na klabu kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 52, lakini rekodi yake ilivunjwal na Pierre-Emerick Aubameyang aliyewasili Arsenal kwa dau la Pauni Milioni 56.
Lacazette alitarajiwa kuingoza safu ya ushambuliani ya Arsenal katika mechi ya Europa League dhidi ya wenyeji, Ostersunds FK, lakini maumivu yanamuondoa.
Mchezaji huyo wa zamani wa Lyon atakosekana pia kwenye fainali ya Carabao Cup dhidi ya Manchester City Uwanja wa Wembley on February 25.
Lacazette alikuwa ana mwanzo mzuri Emirates akifunga mabao manne katika mechi sita za kwanza tangu asajiliwe kuroka Ufaransa, lakini tangu hapo amefunga bao moja tu kati ya 13.