Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema kuwa marekebisho ya katiba nchini Burundi yatazidisha hali ya mtafaruku nchini humo.
Kwa mujibu wa makamu wa rais wa Burundi Gaston Sindimo, Burundi imeskitishwa na matamshi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuingilia kati uamuzi wa taifa huru.
Guterres amefahamisha kuwa kitendo cha serikali ya Burundi kuandaa kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba katika kipindi ambacho Burundi ipo katika mvutano wa kisiasa, mzozo huo utazidi.
Serikali imetoa wito wa maandamano kupinga ripoti iliotolewa na Umoja wa Mataifa Jumamosi.