F Zijuea dawa mbadala 16 zinazotibu uvimbe kwenye kizazi | Muungwana BLOG

Zijuea dawa mbadala 16 zinazotibu uvimbe kwenye kizazi

1. Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu ni chanzo kizuri cha vitamini B6, vitamini C, na madini mengine mhimu ambayo husaidia kuweka sawa homoni za kike.

Sifa yake ya kuondoa sumu mwilini husaidia kuondoa uvimbe kwenye kizazi. Kitunguu swaumu pia huzuia kujitokeza kwa uvimbe wa aina yoyote kwenye mji wa mimba  (uterus).  Tafuna punje 3 za kitunguu swaumu kutwa mara 3.

Kunywa maji glasi moja kila ukimaliza kutafuna kitunguu swaumu kuondoa
ukali na harufu mbaya mdomoni.

2. Juisi ya Limau
Moja kati ya dawa nyingine za asili kwa kuondoa uvimbe kwenye kizazi ni
juisi ya limau.

Ongeza vijiko vijiko vya juisi (majimaji) ya limau na kijiko kidogo cha unga wa baking soda kwenye glasi ya maji ya uvuguvugu, koroga vizuri na unywe mara mbili kwa siku kwa majuma kadhaa.

3. Tangawizi
Mizizi ya tangawizi ni mizuri sana katika kupunguza maumivu na kuongeza
msukumo wa damu.

Andaa chai ya tangawizi (kumbuka ni tangawizi na maji tu, usiweke majani ya chai humo) na unywe kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa majuma kadhaa.

Kwenye hiyo chai tumia asli badala ya sukari kwa matokeo mazuri zaidi. Chai ya tangawizi husaidia kuondoa uvimbe kwenye mirija ya uzazi na kwenye mji wa uzazi kwa ujumla.

4. Mafuta ya zeituni
Moja ya tiba za asili kwa uvimbe kwenye kizazi ni mafuta ya zeituni. Mafuta haya huidhibitihomoni ya  estrogen. Unahitaji kunywa kijiko kikubwa kimoja cha  mafuta ya zeituni sambamaba na juisi ya limau asubuhi mapema tumbo likiwa bado tupu.

Unaweza pia kuandaa  mafuta ya zeituni kwa kuyapika majani ya mzeituni kama
chai ambayo pia husaidia kuongeza kinga ya mwili.

5. Mafuta ya nyonyo
Mafuta ya nyonyo ni mazuri sana kwa kuondoa uvimbe. Weka mafuta ya uvuguvugu ya zeituni kwenye bakuli. Weka kitambaa cha pamba ndani ya hayo mafuta mpaka mafuta yote yanyonywe na yahamie kwenye hicho kitambaa.

Kunja kunja hicho kitambaa na uweke juu ya tumbo ndani ya mfuko wa Rambo na
kisha weka chupa yenye maji ya moto juu yake (ilaze) na uache hivyo kwa usiku mmoja.

Endelea na zoezi hili kwa kila siku kwa siku 5 hivi kisha pumzika kwa siku mbili, rudia hivyo hivyo siku tano kisha siku mbili kupumzika.

6. Maziwa
Maziwa yanasaidia kuondoa uvimbe vizuri kabisa. Maziwa huwa na protini ya kutosha. Kwenye glasi moja ya maziwa ya uvuguvugu ongeza kijiko kimoja cha unga wa giligilani (coriander powder) na kijiko kimoja kikubwa cha unga wa binzari.

Tikisa vizuri mchanganyiko huo na unywe yote. Fanya hivi kutwa mara 2 kwa wiki kadhaa.

7. Unga wa Binzari (manjano)
Sifa ya kimatibabu iliyomo kwenye binzari hupigana pia dhidi ya uvimbe kwenye kizazi. Chukua vijiko vikubwa viwili vya unga wa binzari au unga wa mizizi yake na changanya na maji nusu lita, chemsha kama chai kwenye moto kwa dakika 15, ipua na uache kwa dakika 40.

8. Kitunguu maji
Viuaji sumu (antioxidants) vilivyomo kwenye kitunguu husaidia kuondoa uvimbe kwenye kizazi kirahisi zaidi. Kitunguu pia ni mhimu katika kurekebisha na kuweka sawa homoni za kike.

Kwahiyo kupunguza uvimbe anza sasa kutafuna kitunguu maji kibichi kama kilivyo, usikioshe na chumvi wala maji.