BASF yaanzisha Kiwanda cha uzalishaji kemikali za Ujenzi Dar



Kampuni inayoongoza kwa utengenezaji wa kemikali duniani vilevile kemikali za ujenzi , imeanza kuwekeza madhubuti kwenye uzalishaji wa ndani na hivi leo imekabidhi kituo cha uzalishaji nchini Tanzania. Kiwanda hicho ambacho kitazalisha mchanganyiko wa saruji, kitatumika kupitia makubaliano maalum ya ushuru na kitatoa ufumbuzi wa kibunifu ili kuiwezesha BASF kukidhi mahitaji ya wateja.

Kutokana na kiwanda hicho kipya, kitengo cha kemikali na ujenzi BASF kitajiimarisha katika wigo wa kuwafikia wateja wake wengi zaidi na kukidhi mahitaji ya soko huku ikitoa ufumbuzi wa hali ya juu katika sekta ya ujenzi. "Uwekezaji huu ni hatua nyingine muhimu kwa BASF Afrika.

Ushiriki wetu katika bara la Afrika unaongezeka na jukumu kubwa muhimu linalotekelezwa na kitengo hichi ni kutazama zaidi kwenye nchi zenye mipango mizuri na fursa kubwa, kama vile Tanzania "alisema Michael Gotsche, ambaye ni Makamu wa Rais wa BASF Afrika.

Christian Geierhaas ambaye ni Makamu wa Rais wa kitengo cha kemikali za ujenzi Upande wa Mashariki ya Kati, Asia Magharibi, CIS & Afrika, alisema kuwa "Kuwekeza nchini Tanzania, kutaiwezesha kitengo hicho kuleta bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu na ufumbuzi zaidi kwa wateja wetu katika soko hili muhimu."