Huu ndio muda ambao unatakiwa kurudia kupima tena virusi vya VVU

Baada ya kupata maambukizi, VVU husambaa kwenye damu baada ya siku 4 mpaka siku 6. Baada ya virusi kusambaa,mwili hutengeneza kinga ambayo hujaribu kupambana na virusi . Kinga hii hujitokeza kwenye damu baada ya wiki tatu tangu kupata maambukizi ya VVU.

Kuna Vipimo vingi ambavyo hutumika kubaini iwapo umepata maambukizi. Baadhi ya vipimo hivyo vinauwezo wa kugundua iwapo umepata maambukizi mapema zaidi kuliko vipimo vingine. Vipimo hivi mara nyingi havipatikani katika maabara zetu kutokana na gharama zake kuwa kubwa.

Vipimo vinavyotumika katika maabara zetu huweza kubaini iwapo una maambikizi baada ya wiki tatu toka upate maambukizi. Vipimo hivyo vinategemea iwapo mwili wako umetengeneza kinga. Hivyo unaweza kupima iwapo una maambukizi baada ya wiki 3.

Baadhi ya wagonjwa wakienda katika kipindi hiki cha wiki tatu,vipimo hushindwa kubaini kama wana maambukizi japo wanakuwa na virusi katika miili yao. Hivyo utashauriwa tena kurudia kipimo baada ya miezi mitatu.

Hata hivyo mtu yeyote ambaye ana maambukizi lazima atajulikana iwapo ana maambukizi baada ya miezi sita hata kama vipimo vya awali vilishindwa kubaini maambukizi.
Mpya zaidi Nzee zaidi