Moet & Chandon imetambulisha Rasmi Kinywaji cha Moet Nectar Imperial nchini Tanzania

Balozi wa kinywaji cha kifahari cha Moet & Chandon, Pierre Louis Araud, amefanya ziara yake ya kwanza nchini tanzania wiki hii. balozi huyu ni mtaalamu wa mvinyo na yupo kaztika ziara nchini hapa kwa lengo mahsusi la kutambulisha kinywaji kipya  cha Moet Nectar Imperial na pia kushirikisha wadau. kuhusu kinywaji hiko ulimwenguni.

Akizungumza katika hafla hiyo maalum iliofanyika Hyatt Regency leo, Araud Amesema kuwa urafiki, ushirikiano na ukarimu ni moja kati ya maadili ya chapa ya Moet & Chandon inashiriki katika kuunganisha watu ulimwenguni kote na kujenga urafiki wa kudumu. uzinduzi wa Moet Nectar nchini Tanzania. pia wametaka kureherekea na watanzania kwa kuwa ni marafiki wapya wa Moet na wanaendelea kutoa moyo kwa wale wote wanaopenda kufurahia maisha.

Kinywaji hiko cha Moet Nectar ambapo kinasemekana kina mchaganyiko wa matunda ya kitropiki kama mananasi na maembo, pamoja viungo kama mdalasini na vanila. mchanganyiko wa kinywaji cha Moet Nectar Imperial unajengwa kwa muundo wa zabibu aina mbali mbali ikiwemo aina ya Pinot  Noir (asilimia 40 kwa 50) pia na aina ya Meunier(30 kwa 40)  na pia aina ya Chardonnay kwa asilimia (10 kwa 20). asilimia za matunda hayo yamekamilisha uundaji wa kinywaji hiki na kukiboresha zaidi.