https://monetag.com/?ref_id=TTIb Waziri afika eneo ilipotokea ajali ya moto wa roli | Muungwana BLOG

Waziri afika eneo ilipotokea ajali ya moto wa roli


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Mwigulu Nchemba tayari amefika eneo la tukio ilipotokea ajali ya moto ya roli la mafuta lilitokea katika mlima sekenke na kusababisha vifo vya watu wawili.

Waziri Mwigulu amefika kuangalia jinsi ajali ya gari hilo la mafuta lilivyoanguka na kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu wawili ambao wameungua sana kiasi cha kutotambuliwa hadi sasa huku jitihada zinaendelea kuwatambua.

Kwa mujibu wa shuhuda Edward Lameck, 16,aliyekuwa anapita eneo hilo amesema gari hilo lilifeli break na matairi ya mbele kuanza kuwaka moto hali iliyosababisha gari hilo kutumbukia bondeni na kuwaka moto.

Inaelezwa kuwa imeshindikana watu hao kuokolewa kutokana na kutokana moto mkubwa uliokuwa unawaka. Juhudi zinaendelea kutambua mmiliki wa gari ili kufahamu waliokuwa kwenye gari hilo.