F Zijue dalili, madhara na tiba ya magonjwa ya zinaaa kwa mama mjamzito | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Zijue dalili, madhara na tiba ya magonjwa ya zinaaa kwa mama mjamzito

Magonjwa ya zinaa ni magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana (sexually transmitted diseases),inayosababishwa na bakteria, virus au fungus wanaopenda ishi sehemu zenye maji maji au unyevu unyevu katika mwili kama mdomoni,kooni,sehemu za siri au sehemu ya hajakubwa.

Iwapo mtu atakutana kimwili na mtu mwenye maambukizi hapo ni rahisi kuambukizwa. Magonjwa ya zinaa yanampata mwanamke na mwanaume.

Magonjwa ya zinaa yapo ya aina tofauti kuna Kaswende, Kisonono, Gonorea, Ukimwi, Klamidia, Malengelenge.

Magonjwa ya zinaa ni hatari kwa afya ,mama mjamzito akipata ugonjwa wa zinaa atapata dalili tofauti tofauti kama zifuatazo

Kuvimba sehemu za siri, Maumivu makali pindi ufanyapo mapenzi au wakati wa kukojoa, Kupata homa. Kutokwa vijipele ukeni vinaweza kuuma au visiume, Kupungua uzito, Maumivu ya mgongo, Kutokwa na jasho kwa wingi nyakati za usiku, Kutokwa maji maji ukeni yenye harufu au yasio na harufu, Kutokwa damu au usaha ukeni. Kuwashwa sana au Uke kubadili rangi

Madhara ya magonjwa ya zinaa kwa mama na mtoto

1. Mtoto anaweza kupata upofu

2. Uziwi.

3. Kupoteza kinga za mwili.

4. Kuziba kwa mirija za uzazi.

5. Kifo.

6. Ulemavu.

7. Mwili kudhofu.

8. Kuumwa kwa mara kwa mara.

Tiba
Magonjwa ya zinaa yanatibika iwapo yatatibiwa mapema isipo kuwa ukimwi peke yake hauna tiba, mambukizi mengine mama mjamzito atatibiwa kwa kupewa antibiotic, mtoto  iwapo ataadhirika kipindi mama yake anamimba  baada ya kuzaliwa atawekwa dawa machoni ya kusafisha na kutibu.