Boateng: Hii ndio njia pekee ya kumzuia Ronaldo Bayern vs Real Madrid kesho

Beki wa club ya FC Bayern Munich ya Ujerumani Jerome Boateng amefunguka kuelekea game yao ya nusu fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Real Madrid ya Hispania ambapo game ya kwanza itacheza kesho Jumatano ya April 25 2018 katika uwanja wa Allianz Arena.

Moja kati ya wachezaji ambao wanatajwa kuwa hatari zaidi katika mchezo huo ni staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ambaye amekuwa na wastani mzuri wa ufungaji katika michuano mbalimbali akiitumikia Real Madrid, Boateng akiongea na vyombo vya habari amesema njia pekee ya kumzuia Ronaldo asifunge ni kumzuia kama timu na sio mchezaji mmoja mmoja.

“Njia pekee tunayoweza kumzuia Ronaldo mbele ya goli ni kucheza kama timu, huwezi kumzuia peke yako kabisa, siku zote amekuwa akipata nafasi katika game kutokana na timing yake, hakuna mshambuliaji aliyekamilika zaidi ya Ronaldo kwa sasa, ana uwezo wa kutumia vizuri mguu wa kulia, kushoto na kichwa”- Jerome Boateng