Joyce Banda apanga kurejea Malawi


Leo April 25, 2018 Msemaji wa chama cha Rais wa zamani wa Malawi, Joyce Banda amesema Rais huyo anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi baada ya kukimbilia uhamishoni alikoishi kwa zaidi ya miaka mitatu kwa sababu ya madai ya kuhusika katika rushwa.

Kashfa iliyofahamika kama Cashgate ni ufisadi ulioibuliwa ukiwahusisha maofisa wa ngazi ya juu kwamba walijichotea mamilioni ya dola kutoka hazina ya serikali na ufisadi huo ulifichuka mwaka 2013 wakati akiwa rais.

Wahisani waliamua kukata misaada hali iliyozuia ukuaji wa maendeleo nchini Malawi, moja ya nchi maskini zinazotegemea sana misaada ya kigeni.