Kocha aliyewahi kuzifundisha Kenya , Ivory Coast, Cameroon, Tunisia na Morocco ameaga dunia

Kiungo wa kati wa zamani wa Ufaransa Henri Michel ambaye alikuwa mkufunzi wa mataifa manane wakati wa ukufunzi wake wa miaka 30 amefariki akiwa na umri wa miaka 70.

Aliichezea Ufaransa mara 58 na kuwafunza kutoka 1984 to 1988.

Michel aliiongoza Ufaransa, Cameroon, Morocco, Tunisia na Ivory Coast katika kombe la dunia na pia alikuwa mkufunzi wa timu za mataifa ya United Arab Emirates, Equatorial Guinea na Kenya.

Michel alishinda mataji matatu ya ligi alipoichezea klabu ya Nantes kwa kipindi cha miaka 16

Kazi yake ya ukufunzi ilianza na timu ya taifa ya Ufaransa ambayo ilishinda dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya 1984 mjini Los Angeles .

Pia walifika katika nusu fainali ya kombe la dunia 1986.

Aliajiriwa kuifunza Cameroon 1994; aliifunza Morocco in 1995, UAE 2000, akawa mkufunzi wa Tunisia 2001; kabla ya kuwa mkufunzi wa Ivory 2004.

Michel alirudi nchini Morocco 2007 na baadaye akawa mkufunzi wa Equatorial Guinea na baadaye Kenya.

Alifanya kazi na klabu ya PSG mbali na vilabu vya Afrika ikiwemo Zamalek nchini Misri ,Raja Casablanca ya Morocco, mbali na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini,