4/16/2018

Ndege yalazimika kutua kufuatia abiria kutishia kumchoma peni mhudumu

Kutoka nchini China, mwanaume mmoja anashikiliwa na polisi kwa kosa la kutishia kumchoma na peni mhudumu wa ndege ya Air China jana April 15, 2018.

Polisi wameeleza kuwa mwanaume huyo ametambulika kwa jina Mr Xu, ana umri wa miaka 41. Ndege hiyo iliyokuwa inatoka Changsha kuelekea Beijing ilibidi itue kwa dharura katika jimbo la Henan kutokana na tukio hilo.

Ripoti ya polisi imeonesha kuwa mwanaume huyo anarekodi ya kuwa na matatizo ya akili, jambo linaloweza kumuepusha na adhabu yoyote juu ya tukio hilo.