Serikali ya Israel yatangaza kusitisha kuwafukuza wahamiaji haramu kutoka Afrika


Serikali ya Israel imetangaza kufutilia mbali mpango wa kuwafukuza kwa lazima kutoka nchini humo maelfu ya wahamiaji haramu kutoka barani Afrika.

Serikali hiyo imeandika barua kwenda katika mahakama ya juu zaidi ya Israel na kueleza kuwa suala la  serikali kuwatimua kwa lazima wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika, “sio suala kuu katika ajenda”.

Barua hiyo imeeleza kuwa, maafisa wa uhamiaji wa Israel wanatafuta njia ambayo watawahamisha wahamiaji hao kutoka Afrika kwa hiari.