Watoto 88,000 hatihati kupoteza maisha

Watoto 88,000 wana hatari ya kupoteza maisha kutokana na utapiamlo mkubwa nchini Nigeria.

Ripoti hiyo imetolewa na afisa wa UNICEF.

Kulingana na Afisa Mkuu wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa Geoffrey Ijumba, wakati, watoto 940,000 katika mkoa wa Borno, Adamawa na Yobe wanaathiriwa na njaa, wakati 88,000 kati yao wana hatari ya kupoteza maisha.

"Watu zaidi ya milioni 1.5 hawawezi kupata maji salama katika majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe. Hii inaathiri maelfu ya watoto walio katika kanda," alisema.

Mnamo 2017, UNICEF ilisema kuwa watoto 450,000 chini ya umri wa miaka mitano walikuwa katika hatari ya utapiamlo mkali