Loading...

5/26/2018

Korosho cha chafu za mkoa wa Pwani zahusishwa kuharibu soko la korosho za Lindi

Na Ahmad Mmow, Lindi.
Ili kudhibiti ubora wa soko la korosho zinazozalishwa ndani ya eneo la utawala la chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao.Serikali imeombwa kuimarisha ulinzi katika kizuizi cha Marendego ili korosho chafu zinazotoka mkoa wa Pwani ziingie mkoani Lindi.

Akisoma taarifa ya bodi ya chama hicho wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika leo katika manispaa ya Lindi,meneja ya Lindi Mwambao,Hassan Vudu alisema kutokana na changamoto ya korosho chafu za mkoa wa Pwani kuingizwa mkoani Lindi.Bodi hiyo inaiomba serikali kuimarisha ulinzi katika kituo cha Marendego ili zisiingie mkoani Lindi.

Alisema korosho zinazoingia kutoka mkoa wa Pwani ambazo ni chafu zinapoingia na kuuzwa kupitia vyama vikuu vya mkoa wa Lindi zinaharibu sifa za ubora wa korosho za Lindi.Hivyo kuanza kuhatarisha soko la korosho zinazozalishwa mkoani humo.

Kwakuzingatia madhara yanayosababishwa nakorosho zisizo na ubora kunahaja ya serikali kuongeza uthibiti wa ulinzi katika kizuia hicho katika ukaguzi.Kwani mkazo mkubwa wa ukaguzi unafanywa kwa mazao yanyotoka katika mkoa wa Lindi kwenda mikoa mingine.Lakini ukaguzi wa unaofanywa kuhusu mazao na bidhaa zinazoingia mkoani humu no mdogo.

Sambamba na kuimarisha ulinzi katika kizuia hicho,meneja huyo alisema bodi inaiomba serikali kupitia ofisi ya mrajisi wa tume ya maendeleo nchini kutoa maelekezo na mwongozo kwa viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS)kuweka mkazo kwenye ukaguzi wa korosho kwenye maghala ya AMCOS ikikukabiliana na uchanganyaji wa korosho na mchanga,kokoto,mawe na vitu vingine visivyo hitajika kiasi cha kusababisha kutishia soko la zao hilo kimataifa.

Alibainisha kwamba baadhi ya watendaji,hasa makarani wa AMCOS sio waadilifu.Wanadiriki kuchanganya korosho na vitu visivyo hitajika ili kuongeza uzito.Ikiwa ni njia ya kuficha upungufu  wa uzito wa zao hilo kwenye vyama vyao.

"Changamoto nyingine ni baadhi ya watendaji hawana uwezo wa kutumia kompyuta.Hivyo kudhindwa kuandaa malipo ya wakulima.Kitendo kinachosababisha kuchelewesha malipo ya wakulima,"alisema Vudu.

Alisema kwakuzingatia madhara yanayotokana na watendaji hao kushindwa kutumia kompyuta kinataka wahasibu na makarani kujifunza elimu ya kompyuta.Kwasababu mfumo wa stakabadhi  ghalani umetawaliwa na sayansi na teknolojia.
Loading...