Je mwanao amewahi kupata tatizo la manjano muda mfupi baada ya kuzaliwa. Inawezekana mwanao lakini mtoto wa ndugu yako, rafiki ama jirani yako amewahi kupata tatizo hili. Tatizo la mtoto kuwa na rangi ya manjano ni tatizo ambalo huwaathiri watoto wachanga mara nyingi masaa 24 baada ya kuzaliwa. Tatizo hili kwa lugha ya Kitaalamu hujulikana kama Neonatal Jaundice
Nini husababisha manjano kwa watoto wachanga?
Maradhi ya manjano husababishwa ongezeko la chembe chembe za manjano kwenye damu ya mtoto ya mtoto mchanga. Chembe chembe hizi zinajulikana kwa kitaalamu kama Bilirubin. Ongezeko la chembe chembe hizi hujulikana kama hyperbilirubinemia (kiwango cha juu cha Bilirubin kwenye damu)
Je chembe chembe hizi za manjano hutoka wapi?
Chembe chembe hizi za manjano aina ya Bilirubin hutengenezwa mwilini baada ya chembe nyekundu za damu (red blood cells) kufariki. Watoto wachanga huzaliwa na kiasi kikubwa cha seli nyekundu za damu, hivyo hulazimika kufa ili kuongeza uwezo wa damu kusafirisha oxygen.
Baada ya seli hizi kufa, chembe manjano (Bilirubin) hutengenezwa. Chembe hizi husafirishwa kwenda kwenye ini ili ziweze kubadilishwa na kuongezewa uwezo wa kuyeyuka kwenye maji ili zitolewe nje ya mwili kupitia mfuko wa nyongo kisha kwenye choo kubwa.
Hata hivyo kutokana na uchanga wa ini pamoja na wingi wa chembe manjano, kiasi kikubwa kinaweza kubaki bila kubadilishwa. Kiasi ambacho kinabaki bila kubadilishwa ili kuyeyuka kwenye maji ndio ambacho husababisha mtoto kupata rangi ya manjano.
Chembe manjano (Bilirubin) ambayo inabaki ikiwa na uwezo mdogo wa kuyeyuka kwenye maji ina uwezo mkubwa wa kupenya katika viungo mbalimbali vya mwili ikiwemo ngozi na ubongo.
Nani yuko katika hatari ya kupata manjano?
Hata hivyo mtoto yoyote yule anaweza kupata manjano akiwa mchanga lakini kuna baadhi ya watoto wana hatari kubwa ya kupata manjano kuliko wengine.
Sababu zinazo ongeza hatari hiyo ni kama ifuatavyo:-
1. Rangi / Asili:
Hatari ya watoto kupata manjano ni kubwa iwapo watoto wana asili ya Mashariki ya Kati na Wamerekani wenye asili ya Kihindi. Lakini hatari ni ndogo kwa watoto wenyewe asili ya kiafrika na wamarekani weusi.
2. Ukoo:
Hatari ni kubwa kwa wale watoto wachanga ambao ndugu zao waliwahi kuugua manjano wakiwa wachanga.
3. Lishe:
Hatari ya kupata manjano ni kubwa miongoni mwa watoto ambao hunyonya maziwa ya mama yao na wale ambao hawashibi vizuri.
4. Afya ya mama:
Watoto wanaozaliwa na mama mwenye ugonjwa wa kisukari wako katika hatari kubwa ya kupata manjano.Pia matumizi ya mitishamba kwa mama anaye nyonyesha huongeza hatari ya mtoto kupata manjano.
5. Uzito na Umri wa Mtoto wakati wa kuzaliwa:
watoto wanaozaliwa na uzito mdogo na njiti wako katika hatari kubwa ya kupata manjano.
6.Maambukizi wakati wa kuzaliwa:
Mtoto anayezaliwa na maambukizi yuko katika hatari kubwa ya kupata manjano kuliko yule ambaye hakuzaliwa na maambukizi.
Dalili za Manjano
Dalili za manjano hutokana na uwepo wa rangi ya manjano kwenye ngozi ya mwili na kwenye sehemu nyeupe ya macho. Mara nyingi rangi ya ngozi hutumika ili kubaini iwapo mtoto ana manjano kwa sababu ni vigumu kuiona sehemu nyeupe ya jicho la mtoto mchanga.
Utajuaje iwapo mwanao ana manjano?
Manjano ikiwa nyingi sana inaonekana kwenye ngozi ya mtoto kwa urahisi. Hata hivyo unaweza kufanya hivi ili kuona kama mwanao ana manjano.
Kandamiza kwenye paji la uso la mtoto kisha achia. Iwapo mtoto ana manjano utaona rangi ya njano sehemu uliyokuwa umekandamiza, Pia unaweza kuona kwa urahisi rangi ya manjano kwenye viganja vya mikono na miguu vya mtoto
Madhara ya manjano kwa watoto wachanga.
Kiasi kidogo cha manjano hakina madhara yoyote na huenda kisihitaji matibabu yoyote zaidi ya uangalizi. Hata hivyo mtoto mwenye kiasi kikubwa cha chembe manjano asipopata matibabu ana pata madhara kwenye ubongo. Pia manjano iliyopita kiasi inaweza kusababisha mtoto kupoteza maisha.
Mtoto asipotibiwa anapata ulemavu wa kudumu katika ubongo wake. Hali ambayo hujitokeza kama mtindio wa ubongo, kupooza na ugumu wa kujifunza.
Ufanye nini iwapo mtoto ana manjano
Nenda katika kituo cha afya au wasiliana na daktari wako haraka ili kupata ushauri na maelekezo zaidi kuhusu hali hiyo. Daktari atakueleza iwapo hali hiyo ni ya kawaida au mtoto atahitaji kufanya vipimo ili kuona kiwango cha chembe manjano (Bilirubin) kwenye damu yake.
Matibabu
Iwapo mtoto ana kiwango kikubwa cha chembe manjano daktari wake atamuanzishia tiba mwanga (Phototherapy) pamoja na dawa nyingine ambazo husaidia kupunguza kiwango cha chembe manjano kwenye damu.
Iwapo manjano inatokana na mtoto kutoshiba vizuri mama utashauriwa kumnyonyesha mtoto vizuri na angalau mara nane kwa siku.