6/13/2018

Cannavaro afichua siri ya kutakiwa na Simba


Aliyekuwa Nahodha wa timu ya Taifa Nadir Haroub (Cannavaro) , ambaye ndiye nahodha wa klabu ya Yanga amefunguka kuwa aliwahi kuitwa Simba lakini alishindwa kujiunga kwakuwa mama yake alimkataza.

 Cannavaro amefunguka hayo kupitia KIKAANGONI ya EATV inayorushwa kwenye ukurasa wake wa Facebook, ambapo amesema kuwa alitamani kujiunga lakini hapendi kum kwaza mama yake ambaye hakutaka aichezee klabu hiyo.

“Miaka minne iliyopita Simba SC walishawahi kunifuata nikacheze huko lakini sikukubali ombi lao waliniwekea dola elfu 20, niliacha kusajili Simba SC kwa sababu mama yangu alinikatalia na mimi huwa sipendi nimkere hata kidogo hivyo ikanibidi niende Yanga kujisajili bure mkataba mwingine”, amesema Haroub.

Aidha Cannavaro ameongeza kuwa mbali na kuichezea Yanga pia ni shabiki wa damu wa klabu hiyo na hata akimaliza kuitumikia atabaki hapo hapo.

EATV