Mtalii 'mjinga' apatikana hifadhi ya Serengeti


Mtu mmoja ameelezwa kuwa ''mtalii mjinga ambaye hajapata kutokea'' baada ya kutoa mkono wake na kumpapasa Simba Tanzania.

Picha za video za tukio hilo la ajabu zilionyesha mwanaume huyo akipapasa manyoya ya simba huku akipiga picha kwa kutumia simu yake ya mkononi katika hifadhi ya taifa ya Serengeti nchini Tanzania.

Simba aligeuka haraka akatazama dirisha lililo wazi, kisha akanguruma ishara kuwa yuko tayari kushambulia, watalii waliokuwa ndani ya gari waliruka na kuharakisha kufunga kioo baada ya sauti iliyosikika ikipayuka ''funga kioo''.

Picha hizo zilitolewa kwenye mtandao wa Youtube ukiwa na jina ''Watalii wajinga kupata kutokea'' Watu wengi wakikosoa kilichofanywa na watalii hao.

Inaaminika kuwa simba ambaye awali alionekana kwenye video alikuwa karibu na gari ya watalii akitafuta kivuli.

''Angekuwa na nguvu za kuwavuta watalii kupitia kwenye dirisha na kuwaua papo hapo mbele ya marafiki zao lilikuwa jambo la kijinga sana kufanya''.

''Ilikuwa bahati sana walinusurika simba ni wanyama hatari sana''

''Kama simba angemuua mtu kwenye eneo hilo askari wangepaswa kumuua simba hasa kama angakuwa dume, vinginevyo kungekuwa na madhara makubwa," alieleza Smit.