F Waziri wa afya zanzibar amepokea madaktari bingwa kutoka katika nchi za ulaya | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Waziri wa afya zanzibar amepokea madaktari bingwa kutoka katika nchi za ulaya

Waziri wa afya serikali ya mapinduzi ya zanzibar mhe, Hamad Rashid Mohamed amewataka wafanya kazi katika Tasisi ya matibabu ya Ubongo na uti wa Mgongo (NEURO) kujifunza na kujipatia uzoefu kutoka kwa wataalamu  mbali mbali  wa kigeni  wanaokuja Zanzibar  kwa  ajili ya kutoa mafunzo.

Akizungumza na wataalamu hao katika mkutano uliofanyia katika Hospitali ya Mnazi Mmoja wakati  wa kuwakaribisha kundi la madaktari bingwa wa Uti wa mgongo (NEURO)kutoka nchini marekani, Hispania na Abudhabi ambao watakuwepo zanzibar kwa ajili ya kambi maalum ya matibabu ya maradhi hayo katika Tasisi inayoshughulikia maradhi ya hayo zanzibar.

Amesema “madaktari hao wanaotoka Hospitali kubwa katika nchi zao ni wataalamu wazuri na iwapo wafanyakazi wa Taasisi ya Hospitali ya Mnazimmoja watakuwa wabunifu wanaweza kujifunza mambo mengi kutoka kwao”.

Waziri wa Afya amesema kambi za mara kwa mara za matibabu ya madaktari bingwa kutoka mataifa mengine ni moja ya fursa kwa madaktari wa Zanzibar kujifunza na kuongeza utaalamu wao.

Ametoa ombi maalum kwa madaktari hao wa kigeni kuwashirikisha na kuwafunza madaktari wa kitengo cha NEURO cha Hospitali kuu ya Mnazimmoja  katika operesheni zote watakazofanya.

Aidha amewashauri madaktari hao kufanya utafiti wa kugundua ukubwa wa tatizo la maradhi ya ubongo na uti wa mgongo Zanzibar na kushauri njia zinazoweza kusaidia kupunguza tatizo hilo.

Waziri Hamad amEwataka wananchi wenye matatizo ya Uti wa Mgongo na ubongo kutumia fursa ya kuwepo madaktari hao kwenda kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu bila ya malipo.

Kiongozi wa Madktari hao Prof. Gail Rossean kutoka Chicago Marekani amueleza Waziri wa Afya kuwa wamefurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na Taasisi ya NEURO  ya Zanzibar ya kuwahudumia wananchi na amemuhakikishia wataendelea kuunga mkono juhudi hizo.

Hata hivyo madaktari hao wamesikitika kusikia kuwa hata watoto wadogo Zanzibar wanapata matatizo ya ubongo na uti wa mgongo jambo ambalo sio la kawaida katika nchi wanazotoka.

Hilo ni kundi la nane la Madaktari bingwa wa NEURO kutoka mataifa ya kigeni mwaka huu kuja Zanzibar kwa ajili ya kambi ya matibabu ya maradhi ya Uti wa Mgongo na Ubongo katika Taasisi ya Zanzibar.