WhatsApp yafuata nyayo za Facebook kutumia Kiswahili


Baada ya mitandao ya kijamii maarufu duniani kama Twitter na  Facebook kuitambua lugha ya Kiswahili na kuiingiza rasmi kwenye App zao, na sasa mtandao mwingine wa kijamii wa WhatsApp nao rasmi umeingiza lugha hiyo kwenye App yao.

Kuanzia sasa watumiaji wote duniani wanaovutiwa na Lugha ya Kiswahili watakuwa na uwezo wa kutumia lugha hiyo kwenye App hiyo yenye watumiaji zaidi ya watu bilioni 1 duniani kote.

Mabadiliko hayo ni hatua kubwa kwa lugha adhimu ya kiswahili na huenda ikawa chachu kwa mitandao mingine mikubwa kama Instagram nayo ikaanza kutambua lugha ya kiswahili kwenye App zao.

Jinsi ya kubadili lugha WhatsApp na kuweka kiswahili?

Hatua ya kwanza hakikisha ume-update WhatsApp yako kisha nenda kitufe cha Settings kisha bonyeza Chats na select App Language utakutana na machagulio ya Lugha mbili Kiswahili na Kiingereza na utachagua kiswahili hapo tayari utakuwa umepata WhatsApp yako kwa lugha ya kiswahili.

Hata hivyo, WhatsApp wenyewe hawajaeleza kama mabadiliko hayo ni yale mabadiliko makubwa matano waliyotangaza mwaka jana kuwa watayafanya mwaka huu.